Kibena ni lugha ya Kibantu nchini Tanzania inayozungumzwa na Wabena. Mwaka wa 2001 idadi ya wasemaji wa Kibena imehesabiwa kuwa watu 670,000.
Hii lugha inazungumzwa katika maeneo ya Njombe, Morogoro, Ruvuma na Mbeya.
Kibena ni lugha tajiri sana kwa maneno na ni pana sana ikiwa na lahaja kuu tano: Ki-Kilavwugi (Maeneo ya Ilembula); Kisovi (Kuanzia Lusisi hadi Makambako), Kimaswamu (Imalinyi, Njombe mjini na sehemu ya kata ya Mdandu), Ki-Lupembe (Lupembe) na Kimavemba (Uwemba na sehemu ya tarafa ya Igominyi ambayo si ya Maswamu).
Tunatamani mno kuueneza ujumbe wa habari njema nchini kote Tanzania. Naomba uungane nasi.